17 Mei 2025 - 23:19
Source: Parstoday
Araqchi: Haki ya Iran ya kurutubisha urani kwa malengo ya amani si ya kufumbiwa macho

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba, hakuna sinario na kitu ambacho kitaifanya Iran iachane na haki yake ya kurutubisha madini ya urani kwa malengo ya amani.

Seyyed Abbas Araqchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika ujumbe katika ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa X: Hajapokea pendekezo lolote la maandishi kutoka Marekani liwe la moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Wakati huo huo, jumbe ambazo sisi na ulimwengu tunapokea zinabaki kuwa za kutatanisha na kupingana.

Araqchi amesisitiza kuwa: “Hata hivyo, msimamo wa Iran bado ni thabiti na wa wazi: “Heshimuni haki zetu na hitimisheni vikwazo.” Katika hali hiyo kutakuwa na makubaliano.

Mkuu wa Idara ya Kidiplomasia ya Iran aliendelea kusema: "Ninasema haya kwa uwazi kwamba hakuna hali yoyote ambayo inaweza kuifanya Iran iachane na haki yake ya kurutubisha madini ya urani kwa malengo ya amani, haki ambayo wanachama wengine wote wa Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) wananufaika nayo.

Hivi karibuni pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisisitiza kuwa, urutubishaji wa madini ya urani ukiwa ni sehemu ya mpango wa amani wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu "haujadiliki" na kwamba mazungumzo ya Tehran na Washington hayatazaa matunda ikiwa yatafanyika kwa mashinikizo na bila ya pande mbil kuheshimiana.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha