18 Mei 2025 - 20:33
Source: Parstoday
Guterres: Kuwafukuza watu wa Gaza ni jambo lisilokubalika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, sambamba na kupinga kuhamishwa kwa watu wa Ukanda wa Gaza, amesema kuwa, adhabu ya pamoja dhidi ya watu wa Palestina ni kitu ambacho katu hakihalalishiki.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hayo katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mjini Baghdad siku ya Jumamosi na kueleza kwamba: "Hakuna kitu kinachohalalisha adhabu ya pamoja kwa watu wa Palestina."

Guterres alisisitiza kuwa wafungwa lazima waachiliwe na vita katika Ukanda wa Gaza vikome, na kuongeza kuwa hatukubali kuhamishwa kwa lazima watu wa eneo hilo na tuna wasiwasi juu ya kupanuka kwa operesheni za Israel katika eneo hilo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali pia hatua ya Israel ya kuendelea na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kubainisha kwamba, ujenzi wa vitongoji hivyo ni haramu.

Mkutano wa 34 wa wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu umeanza asubuhi ya leo Baghdad mji mkuu wa Iraq huku kukiwa na migogoro na matukio makubwa katika nchi za Kiarabu na eneo hili.

Wawakilishi wa nchi zote za Kiarabu na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Waziri Mkuu wa Uhispania wanahudhuria mkutano huo wa Baghdad.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha