27 Mei 2025 - 23:38
Source: Parstoday
Mataifa ya Kiislamu yatakiwa yaungane kukabiliana na 'Islamophobia'

Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev ametoa wito kwa mataifa ya Kiislamu kuungana na kusimama bega kwa bega katika kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.

Katika hotuba iliyosomwa kwa washiriki wa mkutano wa kimataifa wa siku mbili huko Baku, wenye mada 'Uislamu katika Darubini: Kufunua Upendeleo, Kuvunja Unyanyapaa,' Aliyev amesema kuwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mwelekeo wa chuki dhidi ya Uislamu, kunafanya iwe muhimu kwa mataifa ya Kiislamu sio tu kuungana, lakini pia kuimarisha mshikamano wao na kupanua uungaji mkono wa pande zote.

"Lazima tusimame kwa mshikamano katika kupambana na chuki dhidi ya Uislamu, ambayo inatesa ulimwengu wote wa Kiislamu, na kupaza sauti zetu kupinga dhulma hii na mienendo hii yenye madhara," Aliyev amenukuliwa akiuambia mkutano huo.

Katika hotuba yake hiyo, Aliyev amesema chuki dhidi ya Uislamu katika miaka ya hivi karibuni imekuwa "wazi zaidi na wa utaratibu" katika kiwango cha kimataifa.

"Uadui dhidi ya Uislamu, chuki na kutovumiliana dhidi ya Waislamu, na hisia dhidi ya Uislamu zinazidi kuenea na kali," Aliyev amesema, akielezea kwamba chuki hizo dhidi ya Uislamu zinajidhihirisha kwa sura mbalimbali.

Aliyev ameeleza bayana kuwa, taasisi kama vile Bunge la Ulaya na Jumuiya ya Mabunge ya Baraza la Ulaya, zinaendeshwa kwa "upendeleo na undumakuwili," na zinachangia kuenea kwa hisia za chuki dhidi ya Uislamu.

Nchi nyingi za Magharibi zimeripoti ongezeko la kutisha la matukio ya chuki dhidi ya Waislamu, hususan baada ya opesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa mnamo Oktoba 7, 2023.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha