28 Mei 2025 - 23:04
Tangazo Maalum | Kutoka Kanisa la Glory Outreach Assembly Tanzania

Ibada kuu na sherehe za kuwekwa wakfu Askofu wa Makanisa ya Glory Outreach Assembly Tanzania. Tukio hili la kipekee litafanyika:Tarehe: Jumapili, 27 Julai 2025.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tangazo maalum: Kanisa la Glory Outreach Assembly Tanzania - Linayo furaha kubwa kuwalika katika: Ibada kuu na sherehe za kuwekwa wakfu askofu wa makanisa ya Glory Outreach Assembly Tanzania. Tukio hili la kipekee litafanyika:

Tarehe: Jumapili, 27 Julai 2025.

Muda: Kuanzia saa 3:00 asubuhi

Mahali: Mji Mdogo wa Lamadi, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu, Tanzania.

Sherehe hii takatifu itaambatana na:

1_Ibada ya kuwekwa wakfu.

2_Huduma ya Neno la Mungu.

3_Nyimbo za sifa na kuabudu.

4_Wageni maalum kutoka ndani na nje ya nchi.

5_Chakula cha pamoja.

Tunawaalika watu wote — viongozi wa dini, waumini, familia, marafiki, na wapenda kazi ya Mungu — kufika na kushiriki tukio hili la kihistoria katika mwili wa Kristo.

“Mtu akitamani kazi ya askofu, atamani kazi njema.”
1 Timotheo 3:1

Karibu tusherehekee pamoja kwa utukufu wa Mungu!

Kwa mawasiliano na taarifa zaidi:
📞 [+255 624 468 558]

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha