Itamar Ben-Gver, Waziri mwenye misimamo mikali wa ndani wa utawala wa Kizayuni jana (Jumatatu) alivamia Msikiti wa Al-Aqswa) wakati wa kumbukumbu ya kukaliwa kwa mabavu Baytul-Muqaddas.
Ben Guer alitekeleza kitendo chake hicho chini ya hatua kali za kiusalama, na baadhi ya wajumbe wa Knesset (Bunge la utawala wa Kizayuni) waliandamana naye katika uvamizi huo.
Wizara ya Waqfu za Kiislamu Quds imetangaza kuwa, sambamba na hatua hiyo, makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa Al-Aqsa huku wakisindikizwa na polisi wa utawala ghasibu wa Israel.
Khatibu na Imamu wa Masjid al-Aqswa amelaani vikali kitendo hicho cha Wazayuni cha kulivunjia heshima eneo hilo takatifu na kueleza kuwa, vitendo hivyo vinavyojeruhi hisia za Waislamu viko wazi sasa kwa kila mtu.
Walowezi wengi wa Kizayuni wenye misimamo mikali mara kwa mara wamekuwa wakivamia msikiti wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu na kufanya vitendo vya kichochezi huku wakiwa wanapatiwa ulinzi na vikosi vya usalama vya utawala haramu wa Israel.
Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.
Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.
342/
Your Comment