Akizungumza pembezoni mwa Jukwaa la Mazungumzo Tehran jijini Iran, Hussein amesema: "Tunahitaji utulivu, usalama, na mchakato wa kisiasa jumuishi Syria. Tunapozungumzia mchakato wa kisiasa jumuishi, tunamaanisha uwepo wa wawakilishi wa makundi yote ya jamii katika mchakato huo, kwani lengo kuu ni kuleta utulivu Syria."
Mwandiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iraq alisisitiza kuwa urejeshaji wa utulivu Syria hauwezekani bila mchakato wa kisiasa jumuishi, kwani mchakato huo unaweza kulinda jamii ya Syria na kuzuia uingiliaji wa kigeni.
"Kuna changamoto nyingi kuhusu suala la Syria. Kwa sasa, vikosi mbalimbali vya kijeshi vimejikita kote Syria: Jeshi la Marekani na vikosi vya Kipalestina viko kaskazini-mashariki, wanajeshi wa Uturuki wanafanya operesheni kaskazini, kambi za Russia ziko katika maeneo ya pwani, na vikosi vamizi vya Israel vinaendesha shughuli katika majimbo ya Sweida na Quneitra."
Hussein amesema: "Mchakato wa kisiasa jumuishi unaweza kulinda jamii ya Syria na kuzuia uingiliaji wa kigeni. Uingiliaji huu wa kigeni hutokea kutokana na migawanyiko ya kijamii."
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Iraq ameongeza kuwa mabadiliko yoyote Syria ni suala la ndani, akisisitiza kuwa utulivu wa Iraq utaathiri kwa kiasi kikubwa hali ya Syria.
Hali ya usalama Syria chini ya utawala wa kundi la Hay'at Tahrir al-Sham (HTS), tawi la kundi la kigaidi la al-Qaeda, bado ni tete. Matukio ya ghasia za kimadhehebu, ikiwemo mauaji ya mamia ya wa kundi la Alawi mnamo Machi, yameongeza hofu miongoni mwa makundi ya wachache kuhusu wapiganaji HTS ambao wanashikilia utawala.
Tangu serikali ya Bashar Assad kuondoka madarakani mwezi Desemba, Syria imekumbwa na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel, ambao sasa umekalia kwa mabavu maeneo makubwa ya kusini mwa nchi hiyo. Pia Syria imekuwa ikilengwa na mamia ya mashambulizi ya anga ya Israel, hasa yakilenga miundombinu ya kijeshi iliyokuwa mali ya jeshi la zamani la nchi hiyo ya Kiarabu.
342/
Your Comment