25 Mei 2025 - 23:03
Source: Parstoday
Kamanda wa IRGC: Iran kwenye vita kamili, lakini nchi iko katika utulivu

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: Tuko kwenye vita kamili, lakini hakuna chochote kinachoonekana kuwa katika hali ya vita; medani za mapambano ziko hai, lakini nchi iko katika hali ya utulivu.

Kamanda huyo mkuu, akizungumza katika hafla ya kuwapongeza mashujaa wa vita vya kujihami vilivyofanyika katika mkoa wa Azarbaijan ya Magharibi, amesema kuwa: "Kile mnachokiona leo kama Iran iliyo huru, yenye mshikamano, yenye hadhi na inayosimama kwa fahari, ni zao la maumivu, jitihada, majeraha, vifungo, kujitolea na kufa shahidi. Yote yametokea katika maeneo  ambayo kila moja linaweza kuchukuliwa kama medani ya Karbala"

Ameendelea kusema: Tumeona hatima ya mataifa ambayo hayakulinda uhuru, umoja na heshima yao kwa wakati unaofaa.

Jenerali Salami ameongeza kuwa: "Tumeona pale adui anapokanyaga ardhi ya taifa fulani, hana huruma kabisa, si kwa watoto, si kwa wanawake wala kwa wazee. Hukata maji, hutumia njaa kama silaha, na hufanya mauaji ya kinyama, huangamiza kila kitu."

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Iran hii tulivu, Iran hii yenye fahari, Iran hii inayotambulika kimataifa kwa jina lake kuu na heshima yake, Iran hii inayosimama imara kutokana na msimamo wake,  yote haya ni matokeo ya jitihada za mashujaa wa vita."

Kauli hiyo ya Jenerali Salami imekuja siku moja baada ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutangaza kuwa, litajibu kwa nguvu zake zote tishio au uchokozi wowote na wala halitaruhusu ndoto za maadui kutimia.

Taarifa hiyo imesema kuwa jeshi, pamoja na vikosi vingine vya jeshi, viko tayari kutetea umoja wa ardhi ya Iran, uhuru, na usalama wa kitaifa, na kwamba kamwe halitawapa maadui wanaojificha fursa ya kutafsiri ndoto zao za fujo kuwa ukweli.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha