Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, Mohammad Eslami amesema hayo katika hauli ya kufa shahidi Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian iliyofanyika jana (Jumamosi) jioni hapa jijini Tehran.
Eslami amesema: Shahidi Amir-Abdollahian alithibitisha kwamba Muqawama na Diplomasia ni kitu kimoja.
Vilevile amesema: "Ni muhimu baada ya kupeana mikono na watu, tupate fursa ya kujifunza kutokana na tabia zao. Uvumilivu na subira ya Shahidi Amir-Abdollahian ilijulikana kwa wote. Katika wakati wa kihistoria tulipokabiliwa na uvamizi mkubwa kwenye eneo hili, tulihitaji aina ya utendaji ambayo Shahid Amir-Abdollahian aliweza kuionyesha."
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran pia amesema: "Ni kanuni ya utambulisho na maadili ndiyo inayoamua tufuate njia ipi na tuunde vipi umoja kwa maslahi ya taifa letu. Kinachopiganiwa na Jamhuri ya Kiislamu ni taifa la Iran kuwa na hadhi na nafasi linayostahiki, kujipambanua katika mwelekeo wake na kusonga mbele katika ufanikishaji wa malengo yake."
Amesema: "Wengine hawawezi kutuamulia tufanye nini. Tunachukua maamuzi na kutenda mambo yetu kwa kuzingatia malengo na maslahi ya taifa letu, hatusubiri idhini ya mtu yeyote."
Eslami pia amesema: "Iran imeweza kudumisha hadhi yake ya kimataifa licha ya usumbufu wote inaofanyiwa na maadui. Kila mtu anakiri haki ya Iran katika nyuklia. Walimwengu wanastaajabishwa na hatua tulizopiga licha ya vikwazo vyote hivi."
342/
Your Comment