Meja Jenerali Mohammad Baqeri amesema hayo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Asim Munir Mkuu wa majeshi ya Pakistan.
Katika kikao hicho sanjari na kumkaribisha Marshal Asim Munir na ujumbe alioambatana nao, Meja Jenerali Bagheri amesisitiza kuwa, shauku na mtazamo wa kistratijia wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa nchi ya Pakistan ni wa kina na wa kudumu.
Amesema, nchi hizo mbili za Iran na Pakistan zimeazimia kuutokomeza ugaidi katika pande zote mbili za mipaka, na uratibu kati ya majeshi ya Iran na Pakistan kuhusu udhibiti wa mipaka umekuwa wa ufanisi na wa thamani, na ushirikiano huu unapaswa kukuzwa.
Meja Jenerali Baqeri amesema, safari ya mwaka jana katika nchi rafiki na ndugu ya Pakistan iliambatana na ukarimu na kumbukumbu nzuri sana, na vikosi vya jeshi vya nchi hizo mbili vinapaswa kudumisha na kuboresha ushirikiano wao wa kijeshi na kiulinzi katika ngazi zote.
Kwa upande wake, Marshal Asim Munir Mkuu wa majeshi ya Pakistan sanjari na kushukuru kwa mapokezi na ukarimu mkubwa wa nchi na vikosi vya jeshi la Iran, amesisitiza juu ya kuimarisha ushirikiano na kuboresha kiwango cha maingiliano kati ya vikosi vya jeshi vya Iran na Pakistan.
342/
Your Comment