Araghchi amesisitizia umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa Iran na Lebanon, wakati wa mkutano wao huo wa jana Jumatano huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon. Iran, waziri huyo amesema, iko tayari kusimama na Lebanon katika "maswala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanayozingatia kuheshimiana."
Sheikh Qassem ametoa shukurani za dhati kwa uungaji mkono wa Iran kwa watu wa Lebanon na Harakati ya Muqawama ya Hizbullah, kwa mujibu wa taarifa ya harakati hiyo. Qassem alichukua wadhifa wa mkuu wa Hizbullah mwaka 2024, baada ya Israel kumuua kiongozi mashuhuri wa harakati hiyo ya Muqawama, Sayyid Hassan Nasrullah.
Sheikh Qassem pia alisisitiza nafasi athirifu ya Iran katika eneo la Asia Magharibi na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kadhia ya Palestina.
Kiongozi huyo wa Muqawama wa Lebanon pia amemtaarifu Araghchi kuhusu juhudi za Hizbullah za kufufua Lebanon, kudumisha utulivu na mamlaka ya ya kujitawala nchi hiyo. Amesema Hizbullah pia inafanya juhudi za kuwafukuza wavamizi wa Israel kutoka ardhi ya Lebanon, imesema taarifa hiyo.
Kwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita ya Novemba 2024 kati ya Israel na Hizbullah, utawala huo ghasibu umeweka wanajeshi katika maeneo matano nchini Lebanon. Jeshi la Israel bado linafanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Lebanon.
Katika mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na Balozi wa Iran huko Beirut Mojtaba Amani, pande hizo mbili pia zilijadili maendeleo ya hivi karibuni ya kikanda, yakiwemo mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel huko Gaza.
Your Comment