Sheikh Naim Qassim amesema, muqawama hauruhusu wavamizi kuweko katika eneo hilo.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, amebainisha kuwa, katika wakati huu muhimu wa kihistoria, ameyataka baadhi ya makundi kuwa pamoja na Hizbullah ya Lebanon na sio kuwa katika safu ya adui.
Kiongozi huyo wa Hizbullah sambamba na kuwakosoa wale wanaotaka kutoa upendeleo kwa adui, amesitiza: "Sio sisi tunaoipeleka nchi kusikojulikana na hatari, lakini watu waliochagua njia hii ni wale wanaotaka kujisalimisha kwa wavamizi na watu ambao wanakodolea macho ya tamaa ardhi yao."
Sheikh Naim Qassim Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, "Tuko tayari kuzungumza nanyi kuhusu masuala yote, na kama kuna jambo ambalo linawatia wasiwasi, tutalitatua. Lakini kamwe msiwe upande wa adui."
Aidha amesisitiza kuwa, "Tuko katika nafasi ya kujilinda, tunasimama dhidi ya adui ambaye ni mvamizi na tumesimama kidete kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi wa Marekani na utawala haramu wa Israel."
Kadhalika Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: "Watu wote ambao ni mabeberu wanafanya njama kutupotosha, lakini hatuna la kufanya zaidi ya kuelekea katika njia sahihi na kudumisha muqawama."
342/
Your Comment