5 Agosti 2025 - 12:44
Maukib ya Dhāfir Abbas Awda (Abu Sayf) kijana kutoka miongoni mwa wakazi wa mji wa Basra, katika eneo la Zurayji

“Kwa sababu ya joto kali la hali ya hewa, tunajitahidi kuwapa wageni sharubati baridi ili wapate nguvu ya kuendelea na safari yao ya ziara.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maukib yake ni ndogo na ya kawaida sana, na iko katika eneo la kiwanda cha karatasi, ambapo yeye hujishughulisha na kuwahudumia mazuwwari kwa kugawa juisi ya limau kavu ya Kibasra (Nuumi Basra).

Dhāfir anasema:
“Kwa sababu ya joto kali la hali ya hewa, tunajitahidi kuwapa wageni sharubati baridi ili wapate nguvu ya kuendelea na safari yao ya ziara.”

Ewe Mwenyezi Mungu Mkarimu na Mwingi wa Rehema!
Tunakuomba uwajalie wale wote wanaofanya khidma kwa ajili yako na kwa ajili ya ridhaa ya Imamu Husayn (a.s), uwalipe kwa fadhila zako zisizo na mipaka — zawadi bora kabisa na neema tukufu zaidi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha