11 Oktoba 2025 - 22:16
Source: Parstoday
Wananchi wa Iran waandamana; waitaka Israel iheshimu kikamilifu makubaliano ya kusitisha vita Gaza

Umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tehran na miji mingine kote Iran jana waliandamana kwa lengo la kuiunga mkono Palestina na kuonyesha mshikamano kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji aidha walitilia mkazo kutumwa haraka iwezekanavyo misaada ya kibindamu eneo hilo lililo chini ya mzingiro. 

Maelfu ya wakazi wa Tehran jana walishiriki katika maandamano kwa jina la Besharat-e Nasr (Tidings of Victory) baada ya Sala ya Ijumaa ambapo walitembea kuanzia maeneo ya Chuo Kikuu cha Tehran hadi katika maidani ya Azadi.

Wakazi wa Tehran walikuwa wamebeba bendera za Iran na Palestina pamoja na picha za makamanda wa muqawama waliouwa shahidi.

Viongozi wa dini, wanafunzi, familia wa mashahidi wa vita na watoto ni miongoni wa watu walioshiriki katika maandamano ya jana ya kuonyesha mshikamano na wakazi wa Ukanda wa Gaza. 

"Mataifa yako macho, tunaunga mkono muqawama, na Palestina itaibuka na ushindi," ni baadhi ya maneno yaliyokuwa yameandikwa katika mabango yaliyobebwa na waandamanaji. 

Maandamano ya kuiunga mkono Gaza yalishuhuhudiwa pia katika miji mingine ya Iran kama Tabriz, Ahvaz, Shiraz, Bandar Ababs, Isfahan na Gorgan. 

Waandaaji wameyataja maandamano ya jana kuwa ni dhihirisho la umoja na mshikamano kwa Wapalestina na kupinga madola ya kibeberu duniani yanayoihami na kuiunga mkono Israel katika vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza. 

Your Comment

You are replying to: .
captcha