Kwa mujibu wa shirika la habari la Abna, likinukuu Al Khaleej Online, viongozi wa GCC, baada ya kumaliza kikao chao cha leo kilichoandaliwa na Bahrain, walitoa taarifa na kusisitiza ushirikiano wa nchi wanachama katika teknolojia na mabadiliko ya kidijitali.
Viongozi wa GCC pia, katika taarifa yao, walitaka kuheshimiwa kwa mamlaka kamili ya nchi sita wanachama na kusisitiza kwamba ukiukaji wowote wa mamlaka kamili ya nchi yoyote mwanachama unachukuliwa kuwa tishio la moja kwa moja kwa usalama wao wa pamoja.
Katika taarifa hiyo, umuhimu wa kukomesha mateso ya Wapalestina ulisisitizwa.
Taarifa hiyo ilielezea kuimarishwa kwa biashara na utalii na kuhimiza uwekezaji katika miradi ya kimkakati, pamoja na kuendelea kufikia maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya kiteknolojia.
Viongozi wa GCC waliendelea kusisitiza juu ya kuimarisha maendeleo ya miundombinu ya kidijitali na kuwezesha biashara ya kielektroniki.
Viongozi wa nchi hizi pia waliona ni muhimu kuunga mkono maendeleo ya mifumo ya pamoja ya malipo ya kidijitali na huduma za wingu (cloud services).
Taarifa hiyo iligusia kuendelea kwa mseto na uimarishaji wa uchumi unaotegemea uvumbuzi na uendelevu, na ilisisitiza jukumu la mazingira na kuimarisha miradi ya nishati safi na mbadala.
Taarifa hiyo ilisema: "Tunasistiza juu ya kuhakikisha utii kamili wa masharti ya makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza, kurahisisha utoaji wa misaada ya kibinadamu na ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza. Tunasistiza juu ya kuimarisha juhudi za kuunda nchi huru na yenye mamlaka kamili ya Palestina ndani ya mipaka ya 1967 na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wake, kulingana na suluhisho la nchi mbili."
Your Comment