Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Baghdad / Washington – Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema imekatishwa tamaa sana na uamuzi wa Iraq wa kujiondoa katika hatua ya kufungia mali za Harakati ya Hizbullah ya Lebanon na Ansarullah ya Yemen, na kusisitiza kuwa itaendelea kuishinikiza Baghdad kuchukua hatua kali.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (ABNA), msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha MTV kuwa Marekani “imesikitishwa sana” na mabadiliko ya msimamo wa Iraq kuhusu hatua hiyo.
Msemaji huyo alidai kuwa:
“Makundi yote mawili yanaweka tishio kwa kanda na dunia.”
Akiendelea kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, msemaji huyo aliyefahamika kwa jina la Tammy Bruce alisema:
“Nchi zinapaswa kuzuia matumizi ya ardhi yao na makundi yanayohusishwa na Iran kwa ajili ya mafunzo, ukusanyaji wa fedha, upatikanaji wa silaha au kutekeleza mashambulizi.”
Aidha aliongeza kuwa:
“Marekani itaendelea kuishinikiza Iraq ichukue hatua za wazi dhidi ya makundi yanayohusishwa na Iran ambayo yanadaiwa kuhatarisha maslahi ya Marekani na Iraq.”
Maelezo ya Uamuzi wa Iraq
Hapo awali, serikali ya Iraq ilikuwa imechapisha kwenye jarida lake rasmi la serikali (Al-Waqa’i Al-Iraqiya) uamuzi wa kufungia mali za taasisi kadhaa, ikiwemo Hizbullah na Ansarullah. Hata hivyo, baadaye kamati inayohusika na kufungia mali ilifafanua kuwa:
1_Kuwekwa kwa majina ya makundi hayo kulifanyika kwa ombi la nje (shinikizo la kigeni)
2_Iraq ilikubali tu kufungia mali za watu wanaohusishwa na ISIS (Daesh) na Al-Qaeda
Hatua hii ndiyo iliyozua hasira na malalamiko makali kutoka kwa upande wa Marekani.
Your Comment