23 Desemba 2025 - 10:34
Source: ABNA
Chombo cha habari cha Marekani chadai familia za wanadiplomasia wa Urusi zinaondolewa Venezuela

Chombo kimoja cha habari cha Marekani kimeidai kuwa Urusi imeanza mchakato wa kuwaondoa familia za wanadiplomasia wake kutoka nchini Venezuela.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la ABNA likinukuu CBS News, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imeanza mchakato wa kuwahamisha familia za wanadiplomasia wa nchi hiyo kutoka Venezuela.

Afisa mmoja wa usalama wa Ulaya ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliuambia mtandao huo: "Hatua hii imechukuliwa kwa sababu ya hali nyeti ya kiusalama."

CBS News ilieleza kuwa wakati maendeleo hayo yakiendelea, miitikio ya kimataifa dhidi ya hatua za hivi karibuni za Marekani kuelekea Venezuela inaendelea.

Katika muktadha huo, Rais wa Brazil, Lula da Silva, katika matamshi yake ya mwishoni mwa wiki iliyopita alionya kuwa uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Venezuela unaweza kusababisha janga la kibinadamu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha