23 Desemba 2025 - 10:35
Source: ABNA
Sheikh wa Al-Azhar: Haiwezekani kuwa upande wowote kuhusu mauaji ya kimbari huko Gaza

Sheikh wa Al-Azhar katika mkutano na balozi wa Italia nchini Misri amesema kuwa mauaji ya kimbari na uhalifu wa utawala wa Kizayuni huko Gaza umefikia hatua ambayo haiwezekani kuwa upande wowote.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la ABNA, Ahmad al-Tayyib, Sheikh wa Al-Azhar, amesisitiza katika matamshi yake kuwa suala la Palestina limefikia hatua hatari ya ukosefu wa haki kiasi kwamba haiwezekani kuwa "neutral" (kutofungamana na upande wowote).

Katika mkutano na Agostino Palese, balozi wa Italia nchini Misri, akiashiria kutokuwepo kwa utashi wa kweli wa kimataifa wa kuchukua suluhu ya mataifa mawili, alisema: "Hakuna hitilafu yoyote kuhusu suala la Palestina, kwa sababu limefikia kiwango cha dhuluma, uvamizi na ukiukaji wa maadili yote ya kistaarabu, kidini, kibinadamu na kimaadili kiasi kwamba haikubali kutofungamana na upande wowote."

Al-Tayyib aliashiria mauaji ya watoto na watu wasio na hatia akisema kuwa hali imefikia mahali ambapo hakuna mtu mwenye chaguo lingine isipokuwa kupinga uhalifu huu au kushiriki katika majanga haya ya kibinadamu.

Aliendelea kusema: "Tumepoteza mashahidi wengi katika uvamizi huu dhalimu na usio wa haki wa Israel, ambao hauwezi kuitwa vita, bali ni mauaji ya kimbari yanayofanywa na jeshi lenye silaha kali dhidi ya watu wasio na ulinzi."

Your Comment

You are replying to: .
captcha