24 Desemba 2025 - 20:59
Iran: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Lakamilisha Majaribio ya Makombora Mapya ya Masafa Marefu

"Uwezo wetu wa kijeshi unalenga kuzuia uchokozi na kulinda mamlaka, ardhi na maslahi ya taifa la Iran"

Iran: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Lakamilisha Majaribio ya Makombora Mapya ya Masafa Marefu

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limefanikiwa kukamilisha majaribio ya makombora yake mapya ya masafa marefu, huku ikitoa onyo kali kwa maadui wake wote dhidi ya kufanya uchokozi wa aina yoyote.

Iran: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Lakamilisha Majaribio ya Makombora Mapya ya Masafa Marefu

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, majaribio hayo yanafanyika katika muktadha wa kuimarisha uwezo wa kujilinda wa Iran na kuimarisha ulinzi wa kitaifa dhidi ya vitisho vya nje. Viongozi wa kijeshi wa Iran wamesisitiza kuwa maendeleo hayo ni sehemu ya sera ya kujilinda, si ya kushambulia.

Iran: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Lakamilisha Majaribio ya Makombora Mapya ya Masafa Marefu

“Uwezo wetu wa kijeshi unalenga kuzuia uchokozi na kulinda mamlaka, ardhi na maslahi ya taifa la Iran,” imesema taarifa hiyo.
Iran imeongeza kuwa itajibu kwa nguvu yoyote jaribio lolote la kukiuka uhuru na usalama wake, ikisisitiza kuwa majeshi yake yako tayari kikamilifu kulinda nchi dhidi ya vitisho vyovyote vya nje.

Iran: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Lakamilisha Majaribio ya Makombora Mapya ya Masafa Marefu

Hatua hii imekuja wakati kukiwa na mvutano unaoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, ambapo Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kuwa haitaanzisha vita, lakini haitosita kujilinda endapo italazimishwa kufanya hivyo.

Iran: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Lakamilisha Majaribio ya Makombora Mapya ya Masafa Marefu

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha