21 Februari 2026 - 21:31
Middle East Eye: Iran ina chaguo za uharibifu mkubwa dhidi ya vitisho +Picha

Kwa mujibu wa uchambuzi wa Middle East Eye, Iran si kama Venezuela katika muktadha wa migogoro ya kikanda, bali ina “kadi nyingi za kucheza” ambazo zinaweza kuwa na athari kubwa za uharibifu dhidi ya adui zake ikiwa mashinikizo ya kijeshi yanazidi kuongezeka. Ripoti inabainisha kwamba Iran inaweza kulenga vituo vya kijeshi vya Marekani katika eneo la Ghuba, ina uwezo wa kutumia nafasi yake katika Strait of Hormuz kama nguvu ya kisiasa au kijeshi, na pia inaweza kufanya mashambulizi yenye nguvu zaidi dhidi ya Israel ikiwa mzozo utazidi kukua

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mhariri mkuu wa tovuti ya habari Middle East Eye katika uchambuzi wake wa hivi karibuni amesisitiza kuwa Iran haiwezi kulinganishwa na Venezuela, na kwamba “ina kadi nyingi za kucheza ambazo ni za uharibifu mkubwa.”

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Iran pamoja na kuwa na uwezo wa kulenga vituo vya Marekani katika nchi zote za Ghuba, pia ina uwezo wa kuifunga Mlango wa Hormuz (Strait of Hormuz) na hata kufanya mashambulizi makali zaidi ya makombora dhidi ya Israel.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha