Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu Al-Masirah, Mohammad Hazimeh, mchambuzi wa Lebanon amesisitiza kuwa matukio ya hivi karibuni yameonyesha wazi kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa nguvu ya kimkakati yenye ushawishi katika eneo na duniani. Mapigano ya hivi karibuni yaliyolenga kuifanya Iran isalimu amri au kuidhoofisha nchi hiyo yameshindwa.
Aliongeza: "Utawala wa Kizayuni leo unachukuliwa kuwa utawala dhaifu unaohangaika kulinda kuwepo kwake na usalama wake dhidi ya nguvu inayoongezeka ya Iran. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejenga upya nguvu zake za makombora na kijeshi. Viwanda vya kijeshi na makombora ya balistiki ya nchi hiyo yameimarishwa, haswa makombora yanayoweza kupenya kwenye mahandaki ya chini ya ardhi."
Hazimeh alibainisha: "Iran inaweza kurusha makombora yake kutoka nafasi mbalimbali, na jambo hili linauweka utawala wa Kizayuni hatarini. Nafasi ya kimataifa na mkakati wa ulinzi wa Iran umeimarika, na vita vya hivi karibuni dhidi ya nchi hiyo vilionyesha kiwango cha nguvu yake ya kijiopolitiki na ushawishi wake kwa usalama wa eneo. Mzozo wowote wa baadaye na Iran utakuwa na gharama kubwa kwa pande chokozi."
Your Comment