Vyanzo hivyo vimeongeza kuwa mazungumzo hayo yanafanyika chini ya usimamizi wa Marekani. Serikali ya Trump inatafuta kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Syria na utawala wa Kizayuni. Inadaiwa pia kuwa mazungumzo hayo yatadumu kwa siku mbili na Tom Barrack, mjumbe wa Trump nchini Syria, na As'ad al-Shibani, waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Jolani, watashiriki pamoja na timu ya Israel.
Vyanzo vya Kizayuni vimeidai kufanyika kwa mazungumzo kati ya Tel Aviv na utawala wa Jolani mjini Paris. Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, chaneli ya 12 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni imevinukuu vyanzo vya Israel vikidai kuwa maafisa wa ngazi za juu wa Syria na wa Kizayuni wanatarajiwa kukutana leo Jumatatu mjini Paris ili kuanza tena mazungumzo kuhusu mkataba wa usalama kati ya Tel Aviv na Damascus.
Your Comment