3 Mei 2026 - 13:49
Source: ABNA
Kuharibiwa kwa Kanisa (Nyumba ya Watawa) na Wavamizi wa Kizayuni nchini Lebanon

Baada ya mwanajeshi wa Kizayuni kumtukana mfano wa Kristo Yesu, sasa vyombo vya habari vya Lebanon vimeripoti kuharibiwa kwa kanisa (nyumba ya watawa) la Wakristo kusini mwa Lebanon na wavamizi wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, vyombo vya habari vya Lebanon viliripoti kuwa utawala wa Kizayuni kwa kutumia tingatinga uliharibu kanisa (nyumba ya watawa) la Wakristo katika kijiji cha mpakani cha Yaroun.

Hili linatokea wakati jeshi la utawala wa Kizayuni linadai kuwa wanajeshi wa Kizayuni waliharibu nyumba katika eneo hili, na nyumba hiyo haikuwa na alama yoyote inayoonyesha kuwa ni mahali pa ibada!

Shirika la kutoa msaada la Kikatoliki nchini Lebanon lilitangaza kuwa wanajeshi wa Kizayuni wameharibu kanisa hili (nyumba ya watawa).

Katika taarifa iliyotolewa na shirika hili imesemekana: Tunaulaani vikali kitendo hiki cha makusudi cha kuharibu mahali pa ibada pamoja na uharibifu wa kimfumo wa nyumba kusini mwa Lebanon, unaofanywa kwa lengo la kuzuia kurudi kwa raia.

Hapo awali, picha za video zilizochapishwa zilionyesha mwanajeshi wa Kizayuni akimtukana sanamu ya Kristo Yesu katika moja ya maeneo ya kusini mwa Lebanon.

Your Comment

You are replying to: .
captcha