Kwa mujibu wa shirika la habari ABNA kwa kunukuu tovuti ya habari "Akka", shirika la redio na televisheni la utawala wa Kizayuni (KAN) lilitangaza kwamba serikali ya Marekani imekabidhi utawala wa Israel hati kuhusu mustakabali wa Ukanda wa Gaza.
Kulingana na ripoti hii, hati hiyo inajumuisha uhamisho wa fedha za Mamlaka ya Palestina kwa kile kinachoitwa "Baraza la Amani".
Pia hati hii inajumuisha kuanza kwa mchakato wa kujenga upya Gaza hata bila kuondoa silaha za Hamas.
Hadi sasa hakuna maelezo zaidi kuhusu hati hii yaliyochapishwa, na maafisa wa Marekani na Kizayuni hawakujibu ripoti hii.
Your Comment