30 Juni 2026 - 18:29
Lariijani: Ushiriki Katika Mazishi ya Shahidi Ni Ishara ya Imani, Utii na Azma ya Taifa

Mwenyekiti wa Baraza la Uamuzi wa Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu ameueleza kuwa kushiriki katika hafla ya kuaga kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni ishara ya imani, utii na azma ya umma uliosimama katika njia ya uhuru, heshima na muqawama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mwenyekiti wa Baraza la Uamuzi wa Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu, Sadeq Amoli Larijani, ametoa wito kwa wananchi wa Iran, mataifa ya Kiislamu na watu wote wanaopenda uhuru duniani kushiriki katika hafla ya mazishi na kuaga Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei.

Amesema kuwa kushiriki katika hafla hiyo si tu kuaga mwili wa kiongozi mkubwa, bali ni kudhihirisha imani, utii na azma ya taifa lililosimama kwa miaka mingi katika njia ya heshima, uhuru na mapambano dhidi ya uonevu chini ya uongozi wake.

Ameongeza kuwa Imam Shahidi aliongoza harakati ya taifa hilo katika misingi ya mshikamano, mapambano na kujitegemea, na hivyo ushiriki wa umma katika mazishi yake ni ishara ya kuendeleza misingi hiyo ya kihistoria na ya kiitikadi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha