19 Julai 2026 - 09:20
Source: ABNA
CENTCOM: Wanajeshi 2 wa Marekani wauawa katika mashambulizi ya Iran

Amri Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) katika taarifa yake ilitangaza: Wanajeshi 2 wa Marekani wameuawa katika mashambulizi ya Iran, mwanajeshi mmoja amepotea na watu 4 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr kwa kunukuu Al Jazeera, Amri Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) ilikiri kwamba majana wanajeshi 2 wa Marekani waliuawa jana nchini Jordan wakati wa kukabiliana na mashambulizi ya Iran.

Katika taarifa iliyotolewa na Amri Kuu ya Jeshi la Marekani kuhusu jambo hili, imeongezwa: Mwanajeshi mmoja wa Marekani nchini Jordan bado amepotea. Wanajeshi 4 wa Marekani walihamishiwa hospitali za Jordan na kisha kuachiliwa.

CENTCOM iliongeza: Wanajeshi wengine walipata majeraha mepesi wakati wa shambulizi la Iran nchini Jordan na walirejea maeneo yao ya kazi.

Hii wakati ambapo kwa kukiri kwa vyombo vya habari vya kimataifa, Amri Kuu ya jeshi la kigaidi la Marekani inaweka idadi halisi ya majeruhi na waliouawa wa wanajeshi wake wakati wa mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran chini ya udhibiti maalum wa kuchujia habari.

Maoni yako

You are replying to: .
captcha