19 Machi 2011 - 20:30

Azizullah Muhammadi, mkuu wa chombo kinachosimamia mashindano ya Ligi Kuu ya Soka ya Iran amesema kuwa, mapato ya mechi za mzunguko wa tano yatapelekwa nchini Somalia katika fremu ya msaada kwa wananchi wa nchi hiyo wanaokabiliwa na baa la njaa.

Ripoti ya ABNA- Azizullah Muhammadi, mkuu wa chombo kinachosimamia mashindano ya Ligi Kuu ya Soka ya Iran amesema kuwa, mapato ya mechi za mzunguko wa tano yatapelekwa nchini Somalia katika fremu ya msaada kwa wananchi wa nchi hiyo wanaokabiliwa na baa la njaa. Dakta Muhammadi amesema, kutokana na wananchi wa Somalia kutaabika na ukame na njaa, chombo kinachosimamia mashindano ya ligi kuu ya soka hapa nchini kimeamua kwamba, mapato yote ya mechi za mzunguko wa tano wa ligi hiyo wiki hii yatakusanywa na kupelekwa nchini Somalia. Amesema kwamba, wanaviomba vilabu vya soka hapa nchini kutoa ushirikiano unaohitajika katika jambo hili la kheri. Mkuu wa chombo kinachosimamia mashindano ya ligi kuu ya soka hapa nchini amesisitiza kwamba, wanamichezo wa Iran kama walivyo wananchi wengine wa nchi hii watafaulu katika mtihani huu na watawasaidia Waislamu wenzao wa Somalia ambao wanaishi katika mazingira magumu mno ya ukame na njaa. Ligi kuu ya soka hapa nchini Iran inaingia wiki yake ya tano huku timu ya soka ya Saba ya Qum na Istiqlal ya Tehran zikiongoza kwa kuwa na pointi kumi.