19 Machi 2011 - 20:30

Abna inatuarifu kuwa: ndege za kivita za marekani zinazoendeshwa kwa mitambo maalum zimeendeleza mashambulizi makali dhidi ya raia madhulumu wa Somalia.

Abna inaendelea kutuarifu kuwa:ndege hizo za Marekani jana Jumamosi zilitupa makombora mengi kwenye maeneo ya mpaka wa Somalia ya Kenya na kuua raia wasiopungua 16.Ndege hizo za Mrekani zimeshambulia vijiji vya Kulbiyow karibu na eneo la Juba ambapo wengi wa wahanga wa mashambulizi hayo ni wanawake na watoto wadogo wa Kisomali.Huku hayo yakiripotiwa, Kenya nayo inaendelea na operesheni zake za kijeshi dhidi ya wanamgambo wa ash Shabab ndani ya ardhi ya Somalia.Kenya inasema kuwa imeamua kuingia kijeshi Somalia kutokana na wanamgambo wa ash Shabab kuhatarisha usalama wa Kenya.Vile vile Mkuu wa Jeshi la Kenya, Jenerali Julius Karangi amesema kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo hawatatoka Somalia hadi pale watakapohisi usalama wa Kenya hauko hatarini.