Brigedia Jenerali Vahidi amesema ndege hiyo ya kijasusi isiyokuwa na rubani ni milki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Tehran ndiyo itakayoamua nini la kufanya kuhusu ndege hiyo iliyokamatwa katika anga ya Iran.Waziri wa Ulinzi wa Iran ameyasema hayo baada ya Rais wa Marekani Barack Obama kuiomba Iran iirejeshee nchi hiyo ndege yake ya kisasa ya kijasusi inayoshikiliwa na jeshi hapa nchini baada ya kushushwa chini kutoka angani kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya vita vya kielektroniki. Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi amesisitiza kuwa Iran ina uwezo mkubwa wa kutengeneza ndege za kisasa zisizokuwa na rubani na kwamba ni miongoni mwa nchi tano duniani zinazoongoza katika uwanja huo.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 284080
ABNA inatuarifu kuwa:Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi amekataa ombi la Rais Barack Obama wa Marekani la kurejeshewa ndege ya kijasusi ya nchi hiyo inayodhibitiwa na jeshi la Iran.