Watu hao wanatuhumiwa na kuhusika na vurugu kwenye uwanja wa Port Said mwezi february mwaka huu wakati wa mechi kati ya timu za Al Masry na Al-Ahly ambapo kulitokea vurugu za mashabiki na watu sabini kuuawa.
Watuhumiwa wote wamekana kuhusika na vurugu hiso wala kusababisha vifo vya mashabiki hao wa soka na wamerudishwa rumande wakisubiri kutajwa tena kwa kesi hiyo ambayo imeasbabisha mashabiki wa timu hizo kutoshuhudia timu zao zikicheza.
Watuhumiwa hao waliingia mahakamani hapo huku waiwa wamevalia nguo nyeupe kama ishara ya kuonyesha hawana hatia na vifo vilivyotokea na kuwapungia mikono mashabiki wenzao wasok waliojitokeza nje ya mahakama hiyo.
Hii leo mahakama kuu imewasomea mashtaka watuhumiwa hao ambao wote kwa pamoja wamekana kuhusika na vurugu zilizotokea.