24 Mei 2012 - 19:30

ABNA inatuarifu kuwa:Maelfu ya wananchi nchi wa utawala haramu wa Israel wamenadamana wakipinga ongezeko la wahajiri wa kiafrika nchini mwao

Maandamano hayo shadidi ambayo yaliongozwa na Michael Ben Ari ambaye ni mbuge kwa tiketi ya  chama cha National Union Part na Ben-Guir na Baruch Marzel ambao ni waandishi wa habari wenye msimamo mkali wa kisiasa.Waandamanaji hao walishika mabango yaloandikwa "Afrika inahitaji misaada si makazi" pia waandamanaji hao walipinga na kuilaumu serikali ya ghasibu ya Benyamin Tetanyahu kwa kudai ya kuwa haijachukua jukumu lolote katika kukabiliana na wahajiri hao.Yafaa kuashiria kuwa utawala ghasibu wa Israel umekuwa ukipokea wahajiri kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Sudan.