Mohammad Baqer Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran, ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Khalid bin Hilal Al-Ma'auli, Spika wa Bunge la Oman, kando ya Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani unaofanyika mjini Geneva, Uswisi.
Sambamba na kushukuru uungaji mkono wa Mfalme na wananchi wa Oman wa kulaani jinai za utawala wa Kizayuni na Marekani katika uvamizi wao dhidi ya Iran, Qalibaf amesema: "kila mtu aliuona huo uaminifu wa Marekani kwa sababu zilikuwa zimefanyika duru tano za mazungumzo, lakini kabla ya duru ya sita tulishuhudia uvamizi dhidi ya nchi yetu".
Spika wa Bunge la Iran ametoa indhari kwa kusema: inapasa wasomi wenye vipawa na viongozi wa nchi za Kiislamu wazione hadaa hizo na utovu huo wa uaminifu na wajue wanakabiliana na kuamiliana na kimelea cha aina gani.
Kwa upande wake, Sheikh Khalid bin Hilal Al-Ma'auli amesema, leo watu wa Geaza wanapoteza maisha kwa njaa, lakini upande wa pili unadai kuwa unatetea haki za binadamu na demokrasia.../
Your Comment