Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limeongeza katika taarifa yake kwamba, jeshi la Israel linalosaidiwa na Marekani na wanakandarasi wake wameanzisha mfumo mbovu wa kijeshi wa kusambaza misaada huko Gaza.
Taarifa hiyo ya Human Rights Watch imesema kuwa mauaji ya Israel dhidi ya Wapalestina wanaotafuta chakula ni uhalifu wa kivita.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeendelea kusema: "Kuendelea Israel kuwanyima misaada Wapalestina ni uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki, likisisitiza kwamba hali mbaya ya binadamu katika Ukanda wa Gaza ni matokeo ya moja kwa moja ya Israel kutumia njaa dhidi ya raia kama silaha ya vita."
Shirika hilo limetoa wito kwa Marekani na Israel kusitisha mfumo mbovu wa ugavi wa misaada huko Gaza, na kuitaka dunia iishinikize Israel kuondoa vikwazo vilivyokithiri na vilivyo kinyume cha sheria vya kuingia kwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Taarifa ya Human Rights Watch imetolewa wakati ambapo vifo vinavyosababishwa na njaa vinaongezeka kwa kasi miongoni mwa raia wa Gaza.
Tangu taasisi ya Wamarekani na Israel ya Gaza Humanitarian Foundation ilipochukua udhibiti wa eti kuingiza misaada huko Gaza, Wapalestina wasiopungua 1,330 wameuawa na wengine zaidi ya 8,800 wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na mabomu ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na wakandarasi wenye silaha wa kampuni ya Kimarekani, karibu na vituo vinavyosimamia zoezi hilo.
342/
Your Comment