Adnan Abu Hasna amesema, watoto wengi wanaozaliwa katika Ukanda wa Ghaza wana uzito mdogo na wafupi kutokana na utapiamlo.
Abu Hasna ameeleza kuwa ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu, mamia ya malori yanayobeba misaada ya kibinadamu lazima yaingie kila siku katika eneo hilo na akaongeza kuwa, utawala wa kizayuni wa Israel unapaswa uhakikishe kunakuwepo na njia salama za kupita malori hayo ya misaada.
Mshauri wa vyombo vya habari wa shirika la UNRWA amesisitiza kuwa msaada huo lazima ufikie moja kwa moja kwenye maghala ya Umoja wa Mataifa ili huko upangiwe utaratibu sahihi wa ugawaji.
Aidha, Abu Hasna amesema, vituo vya kusafisha maji katika Ghaza vimeharibiwa, jambo ambalo limesababisha uchafuzi mkubwa wa maji na kuenea kwa maradhi.
Duru za tiba zimeripoti utapiamlo mkali kati ya watoto wasiopungua 17,000 huko Ghaza, ambapo katika baadhi ya matukio watoto wachanga pia wamefariki dunia kutokana na ukosefu wa chakula, huku kukiwa hakuna mashirika yoyote ya kutetea haki za binadamu duniani ambayo yameweza kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni unaoungwa mkono na Marekani.
Katika taarifa za karibuni zaidi, duru za tiba katika Ukanda wa Ghaza zimeripoti kuwa, watoto wengine wawili wadogo na kijana mmoja wamekufa kwa njaa kutokana na vizuizi vilivyowekwa na utawala wa kizayuni ili misaada ya kibinadamu isiingizwe katika eneo hilo.
Hii ni katika hali ambayo, idadi ya vifo vinavyotokana na njaa sasa imefikia 154, wakiwemo watoto 89.
Takwimu za Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza zinaonyesha kuwa vita vya vinyama na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Ghaza hadi sasa vimeshapelekea kuuawa shahidi Wapalestina wasiopungua 60,249 mbali na wengine 147,089 waliojeruhiwa.../
Your Comment