2 Agosti 2025 - 17:54
Source: Parstoday
Russia: Njia ya sasa ya Ujerumani na Ulaya inauelekeza ulimwengu kwenye Vita vya Tatu vya Dunia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema: "Viongozi wa sasa wa Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya wanageuka kuwa Reich ya Nne, na njia yao ya sasa itauelekeza ulimwengu katika vita vikuu vya tatu."

Katika makala iliyopewa jina la "Maadhimisho ya Miaka 50 ya Makubaliano ya Helsinki: Matarajio, Hali Halisi na Mustakbali" iliyochapishwa katika gazeti la Rossiyskaya Gazeta, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov ameashiria mipango ya Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ambaye ametoa wito kwa wanachama wa EU kutenga Euro bilioni 800 kwa ajili ya gharama za ulinzi na kusema kwamba hali ya sasa barani Ulaya na mwelekeo wa kijeshi uliochukuliwa na nchi za bara hilo unatia wasiwasi sana.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia aidha ameashiria matamshi ya Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, na kuongeza kuwa: "Sambamba na hayo, hivi karibuni Kansela wa Ujerumani alitoa wito wa kuongezwa uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo, kurejeshwa sheria ya ulazima wa kutumikia jeshi la Ujerumani, na kuligeuza jeshi la nchi hiyo kuwa lenye nguvu zaidi barani Ulaya."

Lavrov ameeleza kuwa, hatua hiyo ya Merz inakumbusha njia ile ile ambayo Ujerumani ilipitia kabla ya kuanza Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia na kuongeza: "Hata Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Boris Pistorius ana malengo hayo hayo na ametangaza kuwa yuko tayari kuwaua wanajeshi wa Russia."

Russia: Njia ya sasa ya Ujerumani na Ulaya inauelekeza ulimwengu kwenye Vita vya Tatu vya Dunia

Hapo awali Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orbán alisema kwamba tishio la Vita vya Tatu vya Dunia linazidi kuongezeka na jamii ya kimataifa lazima ifanye kila iwezalo kukizuia vita hivyo.

Your Comment

You are replying to: .
captcha