2 Agosti 2025 - 17:01
Kusambaratishwa kwa Vitengo 3 vya Kigaidi vya ISIS Nchini Libya

Taarifa hii inakuja siku chache tu baada ya kupatikana kwa kiasi kikubwa cha silaha katika ghala moja ndani ya nyumba iliyoko kusini mwa Libya.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Idara ya Ujasusi ya Libya imetangaza kuwa vitengo vitatu vya kigaidi vinavyohusishwa na kundi la ISIS vilivyokuwa vikifanya shughuli katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, hasa kusini mwa Libya, vimesambaratishwa kikamilifu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makundi hayo ya kigaidi yalikuwa na uhusiano na mitandao ya kimataifa barani Afrika na Ulaya.

Afisa mmoja mwandamizi wa usalama nchini humo amesema kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za serikali ya Libya kupambana na ugaidi na kukata vyanzo vya ufadhili wa makundi hayo.

Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zinaeleza kuwa vitengo hivyo vilihusika na kazi za kuandikisha wapiganaji wapya wa ISIS, kuwasafirisha kutoka Afrika Kaskazini kuelekea Somalia na ukanda wa Sahel, kutakatisha fedha kwa kiwango kikubwa, kusaidia wapiganaji waliotoroka kambi ya Al-Hawl nchini Syria kwa kuwapangia makazi ndani ya Libya, pamoja na kusafirisha mali na fedha kwa ajili ya ISIS.

Taarifa hii inakuja siku chache tu baada ya kupatikana kwa kiasi kikubwa cha silaha katika ghala moja ndani ya nyumba iliyoko kusini mwa Libya.

Operesheni hii imeonyesha ukubwa wa hatari ya kiusalama na vitisho vya kigaidi vinavyokumba eneo la kusini mwa nchi hiyo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha