28 Agosti 2012 - 06:19

Mtu mmoja ameuawa na wawili kujeruhiwa, kufuatia sheikh Aboud Rogo wa Kenya aliyekuwa akitoa mawaidha yenye utata, na ambaye anahusishwa na mashambulizi ya kigaidi kuuwa kwa kupigwa risasi. Sheikh huyo aliyekuwa akikabiliwa na makosa kadhaa yanayohusiana na ugaidi katika mahakama za Mombasa na Nairobi, alipigwa risasi karibu 14 kifuani, karibu na barabara kuu inayounganisha Mombasa na Malindi.

Tukio hilo lilisababisha vurugu zilizosababisha watu na makanisa ya huko kuporwa na kuathiriwa. Wakiwa kwenye gari nyeupe, Sheikh Rogo alikuwa ameambatana na mkewe Hania Said na baba yake Abdullah Ali ambaye alikuwa amkekaa kwenye kiti cha mbele. Sheikh Rogo ni miongoni mwa watu watatu wa Kenya ambao serikali ya Marekani inawahusisha na wanamgambo wa kiislamu wa Somalia na kuwawekea vikwazo. Wengine wawili ni Abubaker Sharif Ahmed na Omar Awadh Omar.