Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Kuhudhuria Bw. Ghulam Shabiir kutokea Pakistani katika Masjid Al-Haram na Masjid An-Nabii ilivutia watu wote kutaka kupiga picha nae, na wengi walipiga nae picha za ukumbusho.
Kutokana na habari hii vyombo vya habari vya Saudia Arabia viliandika: Kukusanyika watu mbele ya Mpakistani kutaka kupiga picha nae ilimkasirisha Imam wa Masjid An-Nabii Sheikh Ally Ibn Abdurahman na kutowa fatwa ya kuharmisha kupiga picha zaukumsho na Ghulam Shabiir, Akisema: Kitendo cha kupiga picha ni haramu kwa kua cha poteza hisia ya ibada ya waumini, kwa mantiki hii ni haramu kupiga picha na mtu huyu.
Urefu wake ni mita 2.55, na uzito wake ni kg 170, na jina lake ni maarufu katika miaka ilopita kuwa mtu mrefu duniani na kuvunja rekodi ya dunia na rekodi yake ilithibitiwa katika Kitabu cha Gines.
Hii ni fatwa nyengine ya kuchekesha ya Maulamaa wa kiwahabi, fatwa hii si tu watu wakawaida watacheka bali hata wanazuoni wakiwahabi pia walicheka na kupinga fatwa hii na kuifanyia masihara.
