Hali ya utulivu imetoweka kabisa baina ya Waisrael na waparestina baada ya waisrael kuchoma moto Msikiti wa waparestina ambapo pia vitabu vutukufu vya Qur na vimeteketezwa na moto huo.
Machafuko haya yamewatia hofu waisrael wengi, kitendo cha kuchomwa msikiti imekuwa ni kama kumuamsha zimwi aliye lala, polisi wa Israel wamemuua muandamani mmoja wa kiparestina katika machafuko hayo.
Dunia sasa inaiangalia hali hii kwa macho ya wasiwasi – Je, vurugu hizi za mashambulizi mapya kweli zitaweza kudhibitiwa bila ya kuzuka vita?
Tafauti na Ukanda wa Gaza - ambao kwa miaka kadhaa sasa unashuhudia mapigano yasiokwisha baina ya mashambulizi ya anga ya Palestina wakiwa wanajikinga na mashambulizi makali ya jeshi la Israel. West Bank, Jerusalemu, na miji kadhaa ya kiarabu ndani ya Israeli wao wamekuwa wakiishi kwa utulivu tangu baada ya vurugu za mapinduzi ya pili ya Intifada zilizomalizika mwaka 2005.
Waisraeli kwa mara nyengine tena wanajikuta wakiwa katika hali ya wasiwasi, na hofu ya uwezekano wa kuzuka vurugu kwa mara ya tatu.
Maafisa wametoa wito kuwa umma uwe macho.
Wimbi la ghasia la hivi sasa linatokana na vurugu zilizoanza mwezi wa Juni na Julai mwaka huu. Kufuatia utekaji nyara na mauaji ya vijana watatu wa kiisrael na mmoja wa kipalestina. Vurugu ambazo zilisababisha vita vya siku 50 baina ya Israel na ukanda wa Gaza .
Mshauri wa zamani wa usalama, Yaakov Amidror, jana alijaribu kupunguza wasiwasi wa watu kwa kusema "Bado hatujafikia zile vurugu zilizoleta vuguvugu la mwanzo la upinzani ama Intifada ya mwaka 1987 au lile la pili.”
Lakini kwa upande mwengine mazingira yanaonekana kulingana na yale yaliyosababisha vuguvugu la upinzani wa pili la Septemba mwaka 2000. Wakati huo miongoni mwa sababu ziliyozusha hilo, ilikuwa ni ziara ya kiongozi wa zamani wa upinzani Ariel Sharon katika eneo takatifu la Jerusalem kitu ambacho hakijawapendeza wapalestina.
Na kwa mara nyengine tena eneo hilo takatifu kwa makundi yote mawili waisrael na wapalestina la msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem, limekuwa ndio chanzo cha kuleta vurugu.
Wapalestina wanawashutumu waisraeli kutaka kuvunja makubaliano yaliokuwapo kwa miongo kadhaa sasa, ya kuwa wayahudi wanaweza tu kutembelea eneo hilo lenye msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa, lakini hawana ruhusa ya kusali katika msikiti huo ama eneo hilo.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alikanusha nia yoyote ya kubadili makubaliano hayo.
Aliongeza kwa kusema kuwa wito wa Wayahudi wenye msimamo mkali, wa kutaka haki za kuweza kusali katika msikiti huo wa Al-Aqsa au hata nia ya kuuvunja na badala yake kujenga hekalu la wayahudi hauwakilishi sera za serikali ya Israel.
13 Novemba 2014 - 17:23
News ID: 651238

Hali ya utulivu imetoweka kabisa baina ya Waisrael na waparestina baada ya waisrael kuchoma moto Msikiti wa waparestina ambapo pia vitabu vutukufu vya Qur na vimeteketezwa na moto huo.