14 Novemba 2014 - 11:19
Hatimaye Waparestina wote wapewa ruhsa ya kusali katika masjidil Aqswa

Utawala Ghasibu wa Israel umetangaza kuwaruhusu Wapalestina wa umri wote kuingia na kuswali kwenye msikiti unaozozaniwa wa Al-Aqsa, ruhsa hiyo imekuja kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kwenye mazungumzo ya Jordan, Israel, na Marekani.

Utawala Ghasibu wa Israel umetangaza kuwaruhusu Wapalestina wa umri wote kuingia na kuswali kwenye msikiti unaozozaniwa wa Al-Aqsa, ruhsa hiyo imekuja kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kwenye mazungumzo ya Jordan, Israel, na Marekani.

   Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, ambaye amekuwa kwenye jitihada za kusaka makubaliano ya amani ndani ya kipindi tete cha mzozo wa kisiasa wa kugombania adhri kati ya Israel na Parestina umegeuka  kuwa mzozo wa kidini baada ya Israel kuwafanya matukio kadha wa kadhaa ya kuzuia uhuru wa kidini wa waparestina, amesema hatua kadhaa zimefikiwa katika mkutano baina yake na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pamoja na Mfalme Abdullah wa Jordan, ambao umezungumzia kuhusu kuweka mazingira yatakayosaidia kupunguza mvutano katika eneo la msikiti wa Al-Aqsa.

   Kerry amesema wamekubaliana kupunguza ghasia zinazoendelea kwa sasa na kwamba pande zote zimeahidi kuchukua hatua za kurejesha hali ya utulivu, kwa lengo la kuepusha machafuko yasiyambae zaidi hadi kufika katika hatua ambayo itakuwa ni vigumu kuyadhibiti. Hata hivyo, Kerry hakueleza hatua hizo ambazo zitachukuliwa, ingawa amesema mkutano huo pia unaweza kusaidia katika kuyafufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.

Kabla ya mkutano huo uliowajumuisha viongozi hao watatu, Kerry alikutana na Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas kwa wakati tofauti hapo jana, na pia alikutana na Mfalme Abdullah siku ya Jumatano. Katika mazungumzo yake na Kerry, Mfalme Abdullah alitaka kumalizika kwa kile alichokiita ''vitendo vya uchokozi vya mara kwa mara vya Israel'', katika eneo takatifu.

Aidha, Kerry alielezea yale aliyothibitishiwa na Abbas katika kukabiliana na mzozo huo. '' Rais Abbas ameelezea tena azma yake ya kutaka kutumia njia za amani ili kumaliza ghasia na ametangaza wazi kufanya kila linalowezekana kurejesha utulivu na kuzuia uchochezi wa vurugu na kujaribu kuibadilisha hali iliyopo,'' alisema Kerry.

 Ni Muhimu kuashiria kuwa:Katika wiki za hivi karibuni, ghasia kati ya Israel na Palestina zimepamba moto kwenye mji wa Jerusalem wenye msikiti wa Al-Aqsa, eneo ambalo ni takatifu kwa itikadi ya dini ya kiislamu na kiyahudi. Kumekuwa na hofu kwamba ghasia hizo huenda zikachochea kuzuka kwa vurugu kubwa itakayo keta maafa yasiyozimika kwa haraka.

Israel imekuwa ikifanya jinai mbalimbali dhini ya raia wa Parestina, imekuwa ikiwanyan’ganya nyumba waparestina na kuishi wao, imekuwa ikiwapiga, kuwa funga na hata kuwaua, hatua ya waislael kuchoma masjid na vitabu vitukufu vya waislamu ni hatua ambayo imezua mtafaruku mkubwa mpaka kupelekea waziri wa mambo ya nje ya Marekani kufanya ziara mashariki yakati kwa ajili ya kutafuta Amani na njia ya kuzuia hatari inayosadikiwa kutokea baada ya uchomwaji wa msikiti na vitabu hivyo.

Siku ya Jumatano, Israel iliidhinisha mpango mpya wa ujenzi wa makaazi ya walowezi, mashariki mwa Jerusalem, licha ya ghasia kuzidi kupamba moto. Hata hivyo, mpango huo umekosolewa vikali na Marekani, Jordan pamoja na Palestina.

Wakati huo huo, Israel imeondoa kizuizi cha umri wa watu wanaotakiwa kwenda kuswali kwenye msikiti wa Al-Aqsa. Msemaji wa Polisi wa Israel, Mickey Rosenfeld, amesema leo kuwa wanaume wa rika zote wataruhusiwa kuhudhuria Swala ya Ijumaa, katika msikiti huo ulioko Jerusalem, ambao umekuwa ukigombaniwa, hatua hii inalenga kupunguza hasira za waparestina kufuatia tukio la Israel kuchoma  msikiti  wa waparestina.

Rosenfeld amesema wanategemea kwamba hali itakuwa ya utulivu kutokana na hatua hiyo. Amebainisha kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na mazungumzo yaliyofanyika Jordan kati ya Kerry, Mfalme Abdullah na Netanyahu. Amesema polisi zaidi wamepelekwa Jerusalem leo asubuhi kwa lengo la kuzuia matukio yoyote yanayoweza kusababisha kuvunjika kwa amani kwenye eneo hilo.

Tags