Katika hali ambayo hali ya utulivu bado tete nchini Marekani baada ya polisi mweupe kumuua kijana mweusi, msichana mweusi ambaye ni mjamzito atobolewa jicho huko FERGUSON Marekani.
Msichana huyo ambaye ametambulika kwa jina la Dornella Conners ni raia wa kimarekani mwenye asili ya Afrika anaelezea kuwa walikuwa na rafiki yake kwenye kituo cha mafuta, mbali kidogo na eneo la maandamano ambayo yanalenga kutafuta haki ya kijana mweusi aliyeuawa kinyama na na polisi mweupe.
Dornella Conners anaelezea kuwa baada ya kutoka kituo cha mafuta polisi walituzingira na kutuzuia kwa nyuma na mbele. Rafiki yake alipoanajaribu kutafuta njia ya kutoka ndipo polisi hao walipofyatua risasi za kuzuia maandamano na kumpiga mwanadada huyo mjamzito, katika jicho lake la kushoto, ambapo kwa sasa amepata upofu wa jicho hilo.
Polisi walijitetea kwa kusema kuwa dereva alikuwa akiendesha gari kuelekea waliko hivyo walihisi anadhamira mbaya ya kuwagonga ndipo walipofyatua risasi hiyo.
Mwanadada huyu ambaye kwa sasa amepoteza jicho lake moja aliongea kwa huzuni akisema: kama walikuwa wanania ya kumzuia dereva kuwa gonga mbona hawakumpiga risasi dereva na badala yake wamenipiga mimi niliyekuwa nimekaa pembeni?
Mwanadada huyu aliendelea kusema: nikweli pembeni mwa eneo hilo, kulikuwa na vurugu za waandamanaji, lakini sisi tulikuwa kando na sielewi sababu ya polisi hao kutushambulia sisi.
Mwanadada huyu aliandika katika kurasa yake ya facebuk kwamba: anashukuru yuko hai, na akipata nafuu atafuatulia haki yake