Waparestina wameilaumu Israel kwa kusababisha kifo cha waziri wa nchi hiyo.
Wapalestina leo wameilaumu Israel kwa kifo cha waziri wao wakati wa makabiliano na wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi, wakisema uchunguzi umeonyesha alifariki dunia kutokana na gesi ya kutoa machozi na kipigo. Ziad Abu Ain aliyekuwa na umri wa miaka 55 na waziri asiye na wizara maalum, alianguka wakati wa makabiliano kati ya waandamanaji wa kipalestina na wanajeshi wa Israel jana na akafariki dunia baada ya kuwasili hospitali. Kifo chake kimezusha wasiwasi wa kuzuka upya ghasia katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Jerusalem mashariki, eneo ambalo Wapalestina wanataka liwe taifa lao la baadae. Afisa wa mamlaka ya utawala wa Palestina Hussein al-Sheikh alisema uchunguzi wa kitibabu juu ya kifo cha Waziri Abu Ain, ulifanyika nchini Israel wakiweko wataalamu Palestina, Jordan na Israel, lakini taarifa nyengine zinasema wataalamu wa Palestina na Israel hawakukubaliana juu ya sababu za kifo cha waziri huyo.
Kifo cha waziri huyu kimezua hasira kali sana kwa waparestina wenye misimamo mikali.