5 Januari 2015 - 12:35
Hollande: vikwazo dhidi ya Urusi vinaweza kuondolewa

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema leo kuwa vikwazo vya nchi za Magharibi vinavyoendelea kuiathiri Urusi vinapaswa kuondolewa kama hatua zitapigwa katika ufumbuzi wa mgogoro wa Ukraine.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema leo kuwa vikwazo vya nchi za Magharibi vinavyoendelea kuiathiri Urusi vinapaswa kuondolewa kama hatua zitapigwa katika ufumbuzi wa mgogoro wa Ukraine. Hollande amekiambia kituo kimoja cha redio nchini Ufaransa kuwa anatarajia kupatikana mafanikio katika mazungumzo ya kimataifa yanayopangwa nchini Kazakhstan mnamo Januari 15 katika juhudi mpya za kushinikiza mpango wa amani, ambapo kiongozi wa Ukraine anayeungwa mkono na nchi za magharibi Petro Poroshenko anatarajiwa kukutana na Vladmir Putin wa Urusi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia atahudhuria mkutano huo wa mjini Astana. Hollande ambaye atahudhuria mkutano huo, amesema kuwa wakati bara la Ulaya likiendelea kuyaweka wazi mawasiliano na Putin, ni lazima afahamu ni wapi pa kuweka mstari suala ambalo limemgharimu sana. Vikwazo ambavyo Umoja wa Ulaya na Marekani ziliiwekea Urusi, pamoja na kupungua bei za mafuta, vimefanya thamani ya sarafu ya Urusi kuporomoka kwa asilimia 40 dhidi ya dola mwaka jana.

Tags