Urusi imetoa wito wa usitishaji mara moja wa uhasama mashariki mwa Ukraine leo na kuonya kwamba serikali ya Ukrane, mjini Kiev inatafuta suluhisho la kijeshi katika mzozo huo.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa juhudi za serikali ya Ukraine kutafuta suluhisho la kijeshi katika mzozo huo litaleta madhara makubwa.
Lavrov ameongeza kuwa usitishaji kamili wa mapigano unapaswa kufikiwa haraka iwezekanavyo na kutoa wito kwa mataifa ya magharibi kuitolea mbinyo kile alichokieleza kuwa ni chama cha vita mjini Kiev.
Lavrov anatarajiwa kukutana na wenzake wa Ukraine , Ufaransa na Ujerumani mjini Berlin baadaye leo. Mazungumzo hayo yanaonekana kuwa muhimu kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa nchi nne baadaye wiki hii nchini Kazakhstan.