19 Februari 2015 - 16:05
Ayatulla Sistani asisitiza kushirikiana katika sekta ya mafuta baina ya Iran na Iraq

Kiongozi wa kidini nchi Iraq (Ayatulla Sayyid Sistani) amesisitiza umuhimu wa kushirikiana baina ya Iran na Iraq katika kila upande hasa katika sekta ya uzalishaji mafuta baina ya nchi hizo mbili

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi huyo wa dini ameyasema hayo alipokuwa amekutana na msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  (Ishaaka Jihangardiy) huku akiashiria kushuka kwa bei ya mafuta alisema: kuna ulazima wa kukuza ushirikiano baina ya pande mbili (Iran na Iraq) katika nyanja mbalimbali hasa katika masuala ya uchumi na uzalishaji wa mafuta baina ya nchi hizo
Kiuongozi huyo pia aligusia suala la mabadiliko ya hali ya mashariki ya katika na ulimwengu kwa ujumla nakusisitiza haja kubwa ya kuwepo umoja baina ya mashia na masunni duniani.
Akizungumza katika kikao hicho msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya kutoa ripoti ya uhusiano uliopo baina ya pande hizo mbili alisema: kama yatafanyiwa kazi makubaliano yaliopitishwa baina yetu tutashuhudia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Ishaaka Jihangardiy aliongeza kusema kuwa tumefurahishwa na fatuwa yako ya kusisitiza kukabiliana na makundi ya kigaidi nchini Iraq akimalizia kusema kuwa fatuwa hiyo imeleta mabadiliko makubwa katika muhimili wa mazingira ya amani nchini Iraq na kuiokoa Iraq katika maafa yanayosababishwa na makundi hayo ya kigaidi.