Serikali ya Palestina inapanga kuwasilisha mashtaka ya dhulma walizofanyiwa na serikali ya Israel mara tu baada ya kujiunga na mahakama kuu ya uhalifu ya kimataifa mjini The Hague hapo kesho.
Serikali ya Israel imefanya mauaji na uhalifu wa kivita dhidi ya raia madhulumu wa Palestina, ambapo imeua maelfu ya wapalestina wengi wao ni wanawake na watoto na imebomoa makazi yao na kujenga makazi ya raia wa Israel, dhulma zote hizi zimekuwa zikifanywa na Israel na kutetewa na mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa.
Hata hivyo madai yoyote ya uhalifu katika maeneo yanayokaliwa na waisrael ambayo yalikuwa ni haki ya wapalestina hayatopatiwa majibu kabla ya kupita miaka kadhaa.
Masuala mengine ya kimsingi yatabidi pia yapatiwe jibu.Israel ambayo si mwanachama wa ICC hailazimiki kushirikiana nayo hata kama itashinikizwa na jumuia ya kimataifa ifanye hivyo.