9 Desemba 2016 - 16:33
Al-Jubair: muda si mrefu nitajiuzulu

Mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia ametuma barua ya siri kwa mfalme wa nchi hiyo Salman bin Abdilazizi ikimtaka amtoe madarakani waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Adel Al-Jubair

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamefichuliwa na ukurasa wa Twiteer ambapo Muhammad bin Naif mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia kuwa amendika barua ya siri kwa mfalme wa nchi hiyo Salman bin Abdilazizi inayomtaka kumtoa madarakani waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel Al-Jubeir.
Ombi hilo limetokea baada ya hali ya waziri huyo kushindwa kusimamia wizara yake ipasavyo na mafaili mengi kubaki bila ya kupatiwa uvumbuzi, naye ametoa taarifa ya kujiuzulu kwa baada ya siku kadhaa zijazo huku akisisitiza kuwa mpaka sasa hajapata barua rasmi inayomtaka ajiuzulu.
Mtandao wa Twitter umesambaza picha ya habari hii ambayo pia imesambazwa katika gazeti la Saudi Arabia la “Alwatan” katika Facebook na kusisitiza kuwa: waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia ni muda sasa aonekani katika vikao rasmi vya serikali ya hiyo, ambapo hali halisi inaonyesha kuwa atakae shika nafasi ya waziri huyo tayari ameshapatikana, ambaye ni katika watoto wa familia ya kifalme aliyekuwa karibu sana na mrithi wa ufalme, inasemekana kwamba mfalme wa nchi hiyo atamwainisha atakayeshika nafasi hiyo baada ya kuridi kutoka katika safari zake za vikao vya baraza la ushirikiano wa nchi za Guhaba ya Uajemi.
Adel Al-Jubair alipewa nafasi hiyo na mfalme wa sasa Salman mnamo tarehe 29 mwezi  Aprili mwaka 2015 baada ya miezi mitatu ya kufa kwa mfalme Abdallah nakuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.
Adel al-Jubair ndiye mtu wa kwanza asiyetokana na kizazi cha Saudia kupewa cheo cha uwaziri wa mambo ya nje nchini humo.
mwisho/290