1 Aprili 2019 - 05:25
Waarabu wajadili suala la Syria na Israel

Viongozi wa jumuia ya nchi za kiarabu wamekutana mjini Tunis kwa mkutano wa kilele uliosadifu wakati mmoja na uamuzi wa Rais wa Marekani kuikabidhi Israel milima ya Golan ambayo ni milki halali ya Syria.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Viongozi wa jumuia ya nchi za kiarabu wamekutana mjini Tunis kwa mkutano wa kilele uliosadifu wakati mmoja na uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kuikabidhi Israel milima ya Golan ambayo ni milki halali ya Syria.

Viongozi wa mataifa matatu ya kiarabu, Algeria, Sudan na Moroko wameamua kutoshiriki katika mkutano huo wa kilele wa siku moja uliotarajiwa kupinga uamuzi wa Rais Trump na kuutaja kuwa "batili". Hayo ni kwa mujibu wa rasimu ya taarifa ya mwisho ya mkutano huo wa kilele." Kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa Golan ni ardhi ya Syria inayokaliwa-" amesema hayo mkuu wa jumuia ya nchi za kiarabu Ahmed Abu Gheith mjini Tunis.

"Tangazo lolote na la kutoka nchi yoyote linalokana ukweli huo ni batili kisheria " ameongeza kusema.

Uamuzi wa rais Trump kuhusu Golan ni batil

Uamuzi wa Rais Trump kuhusu milima ya Golan unafuatia uamuzi kama huo alioupitisha mwaka jana alipotangaza kuhamishia Jerusalem kutoka Tel Aviv ubalozi wa Marekani nchini Israel na kuzusha hasira katika ulimwengu wa kiislam.

Rais Bashar al Assad wa Syria hakualikwa kuhudhuria mkutano huo wa kilele . Nchi yake imesitishiwa uanachama kufuatia matumizi ya nguvu yaliyomwaga damu dhidi ya vuguvugu la kudai mageuzi ya kidemokrasi mwaka 2011.

Marekani imekuwa ikizidharau nchi za kiarabu na kudhihirisha bayana kuwa kama si msaada wa Marekani basi nchi za kiarabu zote zingetawaliwa na Iran.

Iran ndio taifa pekee la kiislamu linalopambana na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na washirika wake, pia liko mstari wa mbele kuhakikisha nchi za kiislamu zinapata haki zake. Lakini kwa bahati mbaya asilimia kubwa ya nchi za kiarabu zinasambaza chuki dhidi ya Iran, hii inatokana na ushwawishi wa Marekani.

Mwisho wa habari / 291