(ABNA24.com) Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kwa mara nyingine tena ametaka kurejeshwa ututulivu katika mji mkuu wa nchi hiyo haraka iwezekanavyo.
Ghassan Salame jana alitembelea baadhi ya shule huko Tripoli ambazo zinawahifadhi wahajiri wa nchi ajinabi na kwa mara nyingine tena ametaka kusimamishwa mapigano haraka iwezekanavyo na kurejeshwa utulivu katika mji mkuu huo wa Libya ambao kwa karibu miezi miwili sasa umekumbwa na mapigano makali.
Vituo vya kuwahifadhi wakimbizi katika maeneo yaliyokumbwa na mapigano viko vitupu na sasa wakimbizi hao wamehamishiwa katika baadhi ya shule kutokana na kushtadi mapigano huko Tripoli. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umetoa taarifa na kueleza kuwa Ghassan Salame Mjumbe Maalumu wa umoja huo huko Libya amekagua shughuli zinazofanywa na taasisi za Umoja wa Mataifa katika kutatua mahitaji ya kibinadamu ya wakimbizi hao huko Tripoli. Jamii ya kimataifa imetoa wito wa kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kudhamini usalama wa wakimbizi waliopata hifadhi kwenye vituo mbalimbali huko Tripoli.
Tarehe 4 Aprili mwaka huu Jenerali Khalifa Haftar alitoa amri ya kushambuliwa mji mkuu wa Libya, Tripoli. Jenerali huyo muasi anaungwa mkono na Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), Misri na Ufaransa. Hata rais wa Marekani, Donald Trump alimpigia simu jenerali huyo akitangaza uungaji mkono wake kwa kile alichodai ni kupambana na ugaidi na kulinda usalama wa visima vya mafuta vya Libya.
/129
9 Juni 2019 - 07:40
Msimbo wa Habari: 948517
Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kwa mara nyingine tena ametaka kurejeshwa ututulivu katika mji mkuu wa nchi hiyo haraka iwezekanavyo.