-
Kiongozi wa Mapinduzi: Hatufurutu mpaka katika kuyatazama mazungumzo ya Oman kwa jicho zuri au baya
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, ufuatiliaji ndicho kiungo kinachokosekana katika kufanikisha malengo ya nchi na akasisitiza kuwa ajenda ya pamoja ya mihimili mitatu ya dola ni kufanya jitihada za kufanikisha kaulimbiu ya mwaka huu.
-
Gazeti la US Today: Uchumi wa Marekani umekwama au unakaribia kwenye mdororo
Gazeti la US Today la Marekani limeandika kuwa utabiri unaonyesha kuwa ukuaji uchumi wa Marekani utakabiliwa na mkwamo au unakaribia kudorora licha ya kusimamishwa kwa ushuru wa Trump.
-
Russia: Hatukimbizani na yeyote ili kupata ahueni ya vikwazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amesema katika hali ambayo biashara kati ya nchi hiyo na Marekani imeshuhudia mdororo mkubwa kutokana na "vikwazo haramu vya Washington," lakini Moscow "haikimbizani na mtu yeyote" kwa ajili ya kuondolewa vizuizi hivyo.
-
Viongozi wa Misri na Qatar wakaribisha mazungumzo ya Iran na Marekani nchini Oman
Rais wa Misri na Amir wa Qatar wametoa taarifa baada ya mazungumzo yao huko Doha, mji mkuu wa Qatar na kukaribisha mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani huko Oman.
-
Mkuu wa majeshi ya Israel akiri: Hamas haijashindwa vitani
Mkuu mpya wa jeshi la Israel ameonya kuwa, vikosi vya jeshi la utawala huo wa Kizayuni vinakosa nguvu kazi na rasilimali za kutimiza malengo ya kujitanua ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, na kusema kuwa Hamas inaendelea kuudhibiti ukanda huo, mwaka mmoja na nusu baada ya kuzuka kwa vita hivyo.
-
Idadi ya vifo Gaza yafikia 51,000 huku Israel ikiendelea na mashambulizi ya kinyama
Mashambulizi ya anga ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza yamewaua Wapalestina wengine wasiopungua 17 katika saa 24 zilizopita, na hivyo kufanya idadi ya vifo kutokana na vita vya kinyama vya Israel vilivyoanza Oktoba 2023 kufikia 51,000.
-
Wanachuo wa Iran waendeleza maandamano ya kuiunga mkono Palestina
Wanafunzi, maprofesa, wahadhiri na wafanyakazi wa Vyuo Vikuu vya mikoa ya Ardabil na Khorasan Kusini wamefanya maandamano ya kulaani ghasia na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.
-
Iran: Ufaransa itoe maelezo ya kukamatwa Muirani, mtetezi wa Palestina
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa vikali kitendo cha Ufaransa cha kukataa kutoa maelezo ya kukamatwa Mahdieh Esfandiari, raia wa Iran anayeishi katika mji wa Lyon, kaskazini mwa magharibi mwa Ufaransa, zaidi ya mwezi mmoja baada kutiwa kwake mbaroni na vyombo vya usalama vya nchi hiyo ya Ulaya.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wajadili mazungumzo ya Oman
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudi Arabia wamefanya mazungumzo ya simu na kujadiliana kuhusu uhusiano wa pande mbili na maendeleo ya kikanda na kimataifa.
-
Iran itawapokea wanafunzi na wasomi kutoka vyuo vikuu vya Gaza
Iran itawapokea kwa mikono miwili wasomi na wanafunzi wa Kipalestina katika vyuo vikuu vya Iran kufuatia uharibifu mkubwa wa taasisi za elimu katika Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel.
-
Trump au mkoloni muflisi? Ukosoaji mkali wa mchumi wa Ufaransa dhidi ya sera za Marekani
Gazeti la Ufaransa la "Le Monde" limekosoa sera za serikali ya Marekani katika kuamiliana na nchi nyingine na kuandika: "Mgogoro uliopo si wa kiuchumi tu, bali pia ni mgogoro wa uhalali na utendaji wa kisiasa, unaotokana na uozo wa muundo wa madaraka nchini Marekani."
-
Kuimarishwa biashara kati ya Iran na Eurasia; hatua ya kimkakati
Biashara kati ya Iran na Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Eurasia imekuwa ikistawi siku hadi siku licha ya vikwazo vikubwa vya kiuchumi vilivyowekwa na Magharibi dhidi ya Iran. Kwa mujibu wa tawimu mpya zilizotolewa hivi karibuni, uuzaji bidhaa za Iran kwa nchi wanachama wa umoja huo katika mwaka uliopita uliongezeka kwa asilimia 20 na kufikia karibu dola bilioni mbili.
-
Al_Itarah Foundation | Inatambua thamani na uzito wa Elimu na Maarifa ya Qur'an Tukufu,na umuhimu wa Umoja na Mshikamano wa Kiislamu baina ya Waislamu
Zawadi ya Kiroho na muhimu katika fremu ya kutambua thamani na uzito wa Elimu na Maarifa ya Qur'an Tukufu, na umuhimu wa kuendeleza Umoja na Mshikamano wa Kiislamu baina ya Waislamu.
-
Mheshimiwa Dr. Ali Taqavi, Rais wa Al-Mustafa, Dar-es-Salam -Tanzania, afanya Ziara katika Shule ya Qur'an Tukufu, Zanzibar
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Ziara katika Shule ya Qur'an Tukufu, Zanzibar na tathmini ya Wanachuoni wa Qur'an mbele ya Mheshimiwa Dr. Ali Taqavi, Rais wa Al-Mustafa, Tanzania.
-
Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (S) - Dare-es-Salam, Tanzania, katika Mkutano muhimu na Mh.Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Kaabi
Kufanyika kwa Hafla ya Qur'an Tukufu ndani ya Zanzibar kwa ushirikiano baina ya Jamiat Al-Mustafa - Dares-Salam - Tanzania na BAKWATA
-
Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Iran, Nairobi Dkt. Ali Pourmarjan amtembelea Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Usawa wa Jinsia ya Kenya Mhe. Rehema
Dk. Pourmarjan, mtetezi kwa bidii wa elimu, alieleza dhamira ya Ubalozi wa Iran Nchini Kenya kuwa ni kutoa ufadhili wa masomo kwa Wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu, kwa lengo la kuwapa fursa bora zaidi kwa maisha yao bora ya baadaye.
-
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt Abubakar Zuber Bin Ally atazindua Ofisi Mpya ya Bakwata Kata ya Vingunguti Dar Es salaam.
Ufunguzi huo wa Ofisi hiyo utajiri Kesho Siku ya Jumatano, tarehe 16 April, 2025, Muda wa saa 3 Asubuhi.
-
Siri na Falsafa ya Ratiba ya Darsa ya "Subhi ya Kimaanawi" kwa Wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa, Dar-es-Salam, Tanzania + Picha
Maulamaa wakubwa katika historia zao, walikuwa wakitafuta Adabu (Maadili) kwanza, kisha ndio wanaitafuta elimu. Wengine walikuwa wakiitafuta adabu kwa muda wa miaka 30, na elimu wanaitafuta kwa muda wa miaka 20.
-
Usitishaji vita wa siku 70 huko Gaza; Je, Tel Aviv itakubali na kutii makubaliano hayo?
Mazungumzo kati ya Hamas na Mamlaka ya Misri Mjini Cairo yanaendelea kufanikisha usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza. Makubaliano hayo yanajumuisha kuachiliwa kwa idadi kadhaa ya wafungwa wa Israel na Palestina na iwapo yatakubaliwa, yanaweza kusaidia kuboresha hali ya kibinadamu katika eneo hilo. Walakini, Tel Aviv bado haijajibu vyema kwa makubaliano ya mwisho.
-
Ukisikiliza Qur'an ikisomwa, itakuletea Utulivu wa Moyo na Nafsi | Sikiliza sauti hii nzuri ya kisomo cha Aya ya 260 (Surat Al_Baqara) + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Sikiliza Sauti nzuri ya Tartil ya Qur'an Tukufu. Hakika Qur'an ni Chakula cha Moyo na Nafsi. Kusoma Qur'an Tukufu, na kutafakari / kuzingatia Aya zake, kunaleta Utulivu Mkubwa katika Nyoyo na Nafsi, na kunapelekea kuokoka Duniani na Akhera. Bali tunasema kwamba usomaji wa Qur'an ni Chakula / Lishe Kamili ya Nafsi, na kutapelekea ukuaji wa kimaanawi / Kiroho, na maendeleo ya ukamilifu wa pande zote.