15 Aprili 2025 - 22:12
Source: Parstoday
Viongozi wa Misri na Qatar wakaribisha mazungumzo ya Iran na Marekani nchini Oman

Rais wa Misri na Amir wa Qatar wametoa taarifa baada ya mazungumzo yao huko Doha, mji mkuu wa Qatar na kukaribisha mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani huko Oman.

Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani Amir wa Qatar na mgeni wake Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri wametoa taarifa pambizoni mwa kikao chao cha pamoja ambao wamekaribisha kuendele kufanyika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Washington na Tehran. 

Mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani yalifanyika Jumamosi katika mji mkuu wa Oman, Muscat. Mazungumzo hayo yalihusu kuondoa vikwazo na suala la nyuklia. 

Mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa upatanishi wa Oman, Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Steve Witkoff, Mjumbe Maalumu wa Rais wa Marekani katika Mashariki ya Kati walijadili kuhusu misimamo ya serikali zao kuhusu masuala yanayohusiana na miradi ya amani ya nyuklia ya Iran na kuondolewa vikwazo haramu dhidi ya Iran kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman katika anga chanya na kuheshimiana pande mbili.

Pande mbili  pia zimekubaliana kwamba mazungumzo hayo yataendelea wiki ijayo. 

Katika sehemu nyingine ya taarifa ya mwisho ya kikao chao huko Doha, Qatar, viongozi wa Misri na Qatar pia wamesisitiza kuwa nchi mbili hizo zinaunga mkono kikamilifu mipango ya kuujenga upya Ukanda wa Gaza. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha